Mahojiano
Yuko Ikeda ni mwongozaji mkongwe wa watalii kutoka Japani. Kwa kipindi cha zaidi ya miaka 30 amekuwa akiandaa safari za watalii wa kijapani na kuwapeleka katika nchi mbalimbali duniani ikiwemo Afrika Mashariki. Kwa sasa amestaafu na anaishi mjini Tokyo. Ataelezea tajiriba yake kuhusiana na kazi ya uwongozaji watalii.