3. Vipi unajishughulisha na nini wakati huu? ( Unaendesha mgahawa wa Kikenya
katika eneo la Okayama)
4. Ni kitu gani kilichokuchochea wewe kuanzisha mgahawa wa kikenya. (
Sababu)
5. Ni chakula gani unachopika katika Mgahawa huo ( Biriani, Chai na
kadhalika)
6. Kuna shughuli nyingine ambazo unaendesha kando na kuuza chakula? Meaning
other Activities (Unakusanya Msaada kutoka kwa mtu yeyeto kwa ajili ya
kujenga mahali pa kufanyia mazoezi siku za usoni.)
7. Moyo wako wa kuendesha mgahawa wa kikenya pamoja na ndoto za kutaka
kujenga sehemu ya kufanyia mazoezi katika siku za usoni zinatona na nini?
(Uliwahi kuishi Kenya, sehemu inaitwa Kakamega na historia kidogo ya maisha
yako ulipokuwa Kakamega.)
8. Umeishi kakamega kwa muda gani? (2006- 2008, Kwa mwaka mmoja na miezi
tisa)
9. Katika kipindi hicho ulikuwa unajishughulisha na nini? ( Kufundisha
mchezo wa mpira wa wavu yaani Volley ball kwa maafisa wa polisi na maafisa
wa magereza kila asubuhi)
10. Kutokana na tajriba yako yaani uzoefu wako wa kufundisha mchezo huo,
maoni yako ni yapi kuhusiana na mchezo huo nchini Kenya?
11. Pengine kuna wachezaji wowote wa timu ya taifa ya Kenya ya mchezo huo
unaowakumbuka kwa majina? (Asha Makuto na wengineo)
12. Pengine kuna timu nyingine ambayo umefundisha. (Timu ya vijana ya
sekondari ambayo imeshinda fainali katika michezo ya ????)
13. Ni kitu gani unachojivunia mpaka kufikia sasa. Meaning what you have
achieved so far ever since you opened that restaurant. ( Wanafunzi kutoka
Kenya hutembelea mgahawa, unaendeleza tamaduni ya nchini Kenya pamoja na
kuendeleza uhusiano wa nchi hizi mbili. na mafaniko mengine kama yako.)