mara sauti ikasikika kutoka kichakani ikisema, Tafadhali Kuku usiseme uwongo. buibui alisusihi usimdonoe. alikuwambia kuw aalikuwa akienda nyumbani kwa Mwewe ili akawatibu watoto wake, Lakini wewe hukujali hata kidogo.
buibui alisema hakuwa na kosa lolote kwako. bali tu alikuwa akienda nyumbani kwa Mwewe ili akawatibu watoto wake.
Je,
unakumbuka ulivyomjibu?
Kuku na Mwewe walishangaa kusikia sauti ile kutoka kule kichakani.
kuku akauliza, je, wewe ni nani mwenye kilimilimi? Wadakiaje mazungumzo ya watu?
Kwanza wewe unahusika vipi na mazunmuzoyetu?
kabla ya swali la kuku kujibiwa, kile kichaka kilitikisika kidogo. mara akatokea panzi.
Akaruka kwa nguvu na kutua walipokuwa Mwewe na kuku.
wote wawili walishituka sana.