Mwanariadha wa Kenya Samwel Kimani amejishindia medali ya kwanza ya dhahabu katika michezo ya Olympiki ya walemavu -Paralympiki 2016 …katika baada ya kushinda mbio za 5000m kwa wanaume wasioona
Odair Santos wa Brazil alishinda medali ya fedha , huku ,Erick Sangwa Kenya akishinda medali ya shaba
Licha ya kwamba Waingereza wengi wamefanya vizuri tayari, lakini kwa Lorraine Lambert na mshirika wake katika mchezo wa kulenga shabaha Karen Butler wameshindwa kufuzu kwa fainali za wanawake mita 10 kulenga shabaha.
Kenya ilishinda medali mbili za dhahabu katika Olympiki ya walemavu ya mwaka 2012 mjini London na medali 6 kwa ujumla.