KATIKA KUSIKILIZA KWANGU MASOMO YA BISHOP GWAJIMA.
NIMEJIFUNZA MENGI
HAYA NI BAADHI YA MANENO YAMENIGUSA NA KUNIFANYA NIZIDI KUKUA KIROHO.
NIMEPENDA TUJIKUMBUSHE,
NINANUKUU:
KATIKA MAISHA HUWEZI KUMUONA MUNGU ILA PALITOKEA MTU AMETUMWA KUTOKA KWA MUNGU JINA LAKE YOHANA.
Imeandikwa:
Hakuna aliyemuona Mungu akaishi.ispokuwa mwana pekee.
Ndio maana hata Yesu alipokuja Duniani alivaa mwili angekuja katika Roho tungekufa wote.
Palitokea mtu ametumwa jina lake Yohana.
Mungu ana kawaida ya kuwatuma watu hapa duniani,anawatuma watu ili waseme kwa niaba ya Mungu.Wazungumze kama sauti ya Mungu.
Ukisikia maneno yao umesikia maneno ya Mungu,Ukiasi maneno yao umemuasi Mungu.
Lakini unaweza kumkuta mtu bila kujua,Anabishana na maneno ya mtu wa Mungu,akiwaza kwamba nitabishana naye nitaenda kusoma Bibilia harafu maana hata mimi Bibilia naijua nitakubaliana naye.Akiwaza ni Mtu anayeniambia.
Sikiliza nikuambie,Mfalme sedekia akaambiwa na Yeremia akisema tubu,tubu tubu, utachukuliwa utumwani,usipotubu utachukuliwa utumwani.
Mfalme sedekia akasema hakuna sichukuliwi utumwani hapa.baada ya miaka majeshi ya Mfalme babeli yakamzunguka,wakati huo Yeremia kwasababu amemuonya sana anamkera mfalme , Tuatakatwakatwa tutatobolewa macho mfalme sedekia akakerwa na kumuweka gerezani.
Baada miaka mingi Yeremia amefungwa,wakasikia babeli imekuja imezunguka yelusalem,mfalme akasema haya ni maneno ya Yeremia hayatatokea.
Akatuma ujumbe kwa mfalme wa misri(farao) mfalme wa misri alikuwa na jeshi kubwa,akamwambia njoo unisaidie kupigana na mfalme wa babeli,akiamini mfalme wa misri ana jeshi kubwa yale maneno aliyoyasema Yeremia hayatatimia.
Basi kweli wababeli wakasikia mfalme wa misri anakuja kumsaidia mfalme wa islaeli,
Yeremia akatabiri tena akisema kama Bwana aishivyo mfalme wa misri hatakuja kukusaidia na akarudi nyuma.
Yale mabwana yakasikia Na yakavunja ukuta yakamkamata mfalme na wengine wakamuoka kwenye moto.
Yeremia akatabiri mtachukuliwa utumwani
Manabii wengine ndani ya izilael wanatokea wanasema
Bwana asema jitiieni moyo hakuna litakalo wapata,
Na hawa manabii wanajiita wa Mungu,wanaompinga yeremia.
Yeremia anasema mtatiwa utumwani,nabii hanania anasema kama Bwana aishivyo kama vile ninvyovunja nira hii ndivyo hii ndivyo utakavyoivunja nira ya babeli.
Akatokea Yeremia amevaa nira shingoni mwake anatokea nabii mwingine anaikamata nira ya Yeremia na kuivunja na kusema kama Bwana asema kama ninavyoivunja nira ya Yeremia ndivyo utakavyoivunja nira ya mfalme wa babeli.
Yeremia anarudi Nyuma Mungu anamwambia wale manabii ni wa uongo rudi ukatabiri,Yeremia anasema kama vile ulivyoivunja nira ya mti ndivyo Bwana atakutengenezea nira ya mpya chuma.
Tunajifunza kuwa kwenye Bibilia kumbe kuna mtumishi wa Mungu anaweza kuongea maneno ya kuonya,maneno yenye kuongoza halafu anapatika mwingine mahali anawatumainisha watu kwa maneno ya uongo.
Mungu akamwambia Yeremia waache manabii wawatumainishe maneno ya uongo.wataokwa na mfalme wa babeli pamoja na mfalme wao.
HAKUNA FURAHA KATIKA DHAMBI.MTU ASIKUTUMAISHE LOLOTE KATIKA DHAMBI NI KUTUBU.
Aonywaye mara nyingi akashupaza shingo yake itavunjika ghafla naye hata pata Dawa.
Soma .
Yona 3:1-10
Bibilia inasema afichaye Dhambi hatafanikiwa bali yeye aungamae na kuziacha atafanikiwa.
Utakapoitikia ukasema naamua kutubu,kughaili,naye Mungu ataghaili mabaya aliyopanga kuyaruhusu,
Kabla Mungu hajakupiga huleta maonyo.
Kuna watu wasingevuka 2015,ukiwa kazini,ukiwa mzima,ukiwa na macho yote,
Zitafakalini njia zenu.
Mwonyeshe Mungu mahali ulipokosea.
Zaburi 103:3,12
1Yohana 1:7
1 yohana 1:9
NAWATAKIA USIKU MWEMA.