KANUNI ZA MATUMIZI
Kwa kujisajili na 8gear.jp(hapa itaitwa tovuti) Utakuwa una thibitisha kuwa umesoma na kukubali kufuata sheria na masharti za kuitumia tovuti hii. sheria na masharti haya(Hapa yatatajwa kama makubaliano ya mtumiaji) yatakuwa yanajumuisha uwajibikaji wako kisheria kwa 8Gear( hapa ikitajawa kama 8gear.jp, au sisi). Makubalino ya mtumiaji yatatumika pale mtumiaji mpya, anapo kubali na kujisajili kutuimia. 8Gear inaweza kubatilisha makubaliano hayo kwa kuweka mabadiliko kwenye tovuti. Mabadiliko yatachukua mkondo moja kwa moja baada ya siku 30, ambapo matumizi yote yatatawaliwa na mabadiliko hayo mapya. Maanake ni kuwa unashauriwa kuangalia mara kwa mara iwapo kuna mabadiliko kwenye makubaliano ya mtumiaji. Iwapo sehemu fulani ya makubaliano itapatikana kuwa batili, utupu au kwa sababu yoyote haiwezi kutekelezwa, basi sehemu hiyo haitatatiza utekelezaji au uhalali wa sehemu nyingine ya makubaliano ya mtumiaji.
Kipaumbele:Maneno au vishazi vilivyo pigwa mistari ni viungo vya kurasa na tovuti nyingine. Na kwa kukubali sheria na masharti yaliyoko kwenye makubaliano ya mtumiaji, , ina maana kuwa matumizi ya tovuti nyingine tanzu itatawaliwa na makubaliano ya mtumiaji na sera ya faragha iliyochapishwa kwenye tovuti hiyo.