HOTUBA YA DKT. BATILDA S. BURIAN, BALOZI WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA KWENYE MASHINDANO YA KISWAHILI YATAKAYOFANYIKA CHUO KIKUU CHA SOKA, JUMAPILI TAREHE 22 NOVEMBA 2015.
Mhe. ….,
Waheshimiwa Mabalozi,
Wawakilishi wa Mabalozi,
Majaji wa Shindano,
Mabibi na Mabwana
Wanafunzi wa Chuo Kikuu Cha Soka,
Ninafuraha sana kusimama hapa mbele yenu kwa mara ya kwanza. Mimi ni Dkt. Batilda Salha Burian, Balozi wa Tanzania nchini Japan. Mnaweza kusema bado ni mgeni kwa sababu ni miezi 7 tu tangu nimefike kwenye hii nchi yenu.
Niliposikia kwamba kuna mashindano ya lugha ya Kiswahili nilifurahi na kushangaa sana, sikutegemea kama nitakuta watu wenye hamu ya kujifunza Kiswahili huku mbali, kwa hiyo nilipoaalikwa kuja hapa leo sikusita hata mara moja.
Mabibi na Mabwana,
Lugha ni kiunganishi kikubwa sana katika jamii tofauti, kwa sababu inaleta maelewano. Na maelewano huleta umoja na amani. Lugha ya Kiswahili ni lugha ya kujivunia sana barani Afrika kwa sababu ni lugha yetu wenyewe, tofauti na nyingine kama, kiingereza, kifaransa, kireno au kiarabu. Kama mnavyofahamu Kiswahili kinazungumzwa Tanzania, Kenya, Jamhuri ya Demokrasia ya Kongo, Burundi, Rwanda, sehemu za Somalia, Uganda, Zambia, Malawi, Msumbiji mpaka Visiwa vya Comoro.
Mabibi na Mabwana,
Shindano la mwaka huu linahusu “MWAKA WA AFRIKA”, hii ni sahihi kabisa. Takwimu zote duniani kwa mwaka huu zinanonyesha hamna sehemu yeyote duniani ambapo uchumi wake unakua kama Afrika. Uchumi wa nchi zilizoendelea unaporomoka na kusuasua lakini nchi za Afrika Uchumi wake unaendelea kupaa. Uchumi wa Bara la Afrika unakua kwa asilimia 5 hadi 8 kwa mwaka.
Bara la Afrika ndio bara lenye vijana wengi kuliko yote duniani ifikapo 2040 itakua na nguvu kazi ya watu bilioni moja. Bara la Afrika ni bara lilojaliwa rasilimali zote hapa duniani.
Kuna vivutio vya kiutalii vingi sana Afrika kama mlima Kilimanjaro nchini Tanzania, Victoria Falls mpakani wa Zambia na Zimbabwe, jangwa la Sahara Afrika Magharibi na Kaskazini, kuna jangwa la Kalahari Afrika ya Kusini.
Pia madini na vito vyote vinapatikana Afrika kama almasi, dharabu, Tanzanite, chuma, makaa ya mawe, na madini mengine mengi tu.
Mabibi na Mabwana,
Tunaelewa Bara la Afrika bado lina viunzi na mitego mingi yakupitia mpaka lifikie hatua za Nchi zilizoendelea kama Japan. Lakini kwa kushirikiana kwa pamoja tunaweza kusonga mbele nakuaachana na umaskini.
Wakati umefika kwa watu duniani kuacha kuliangalia bara la Afrika kama sehemu yenye vita, maradhi na umasikini wa kutupa.
Mabibi na Mabwana,
Kwa kumalizia nachukua fursa hii kukishukuru Chuo Kikuu Cha Soka kwa kuandaa tena mashindano haya na ninasuburi kwa hamu sana kusikiliza nsha za wanafunzi wa mwaka huu. Na ninawatakieni wote mashindano mema.
AHSANTENI KWA NISIKILIZA