akamuuliza kuku, hicho mnachokula ni nini? Mbona miguu yake inafanana na ile ya buibui?
Kuku akajibu, Ndiyo, huyu ni buibui.
Mwewe akaona uchungu sana, akasema, Loo!Rafiki yangu, mbona umemuua mganga wa watoto wangu?
Kuku akasema,
hivi wewe bado unaamini waganga? Mimisiwaamini. Waganga wote ni matapeli tu. Hata hivyo, Buibui hakuniambia kama alikuwa anakuja kuwatibu watoto wako.
Kwa hiyo, nikamuua na kumla pamoja na watoto wangu! kuna ubaya gani?