Watoto wanne wamefariki dunia baada ya nyumba waliokuwa wamelala kuteketea kwa moto.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma, Lazaro Mambosasa amesema jana kuwa tukio hilo lilitokea usiku wa kuamkia jana katika Mtaa wa Nyerere kwenye Mji Mdogo wa Kibaigwa Wilaya ya Kongwa mkoani hapa wakati mtu aliyeachiwa kuwaangalia watoto kuwafungia ndani na kwenda baa.