Majibu.
1: Mimi Ninaitwa Mitsuru INOUE. Ninaishi katika mji wa Okayama, magharibi mwa Japani.
2: Nimejifunza lugha ya Kiswahili kwa kipindi cha miaka -------
Kwanza nilikuwa na mwalimu aliyenifundisha Kiswahili hapa Japani kisha……………
3: Kwa sasa hivi nimefungua mgahawa katika eneo la Okayama ambako ninaishi karibu na kituo cha treni cha Okayama. Sasa ni miaka ………….kutoka nilipofungua mgahawa huu. Wateja ninaowahudumia ni wenyeji ambao hawajui kuzungmza Kiswahili, wale wanaotaka kujifunza lugha hii hata na wale ambao tayari wanaifahamu.
4: Mimi nilifanya kazi na shirika la ushirikiano wa kimataifa la Japani yaani JICA kuanzia mwaka wa 2006 hadi 2008 kama mfanya kazi wa kujitolea. Baada ya hapo, nilianza kufiria ni namna gani ambayo ninaweza kurudisha asante kwa nchi hii ambayo niliipenda. Ndio nikaamua kufungua Mgahawa huu.
5: Ninapika Biriani, chai na vilevile kinywaji cha bia ya Tusker kinapatikana.
6. Nilijifunza kupika biriani nchini Kenya………Nilichukua muda wa miaka kujifundisha.
7: Ndoto yangu ya baadaye ninataka kufungua uwanja wa kufanyia mazoezi kwa wachezaji wa mpira wa wavu.
8: Kwa sababu nilipokuwa Kenya niliishi sehemu inayofahamika kama Kakamega kwa kipindi cha mwaka mmoja na karibu miezi 9. Pia nikaishi Ruiru kwa miezi miwili. Katika eneo hilo nilipata nafasi ya kufundisha timu ya voliboli ya askari wa magereza ambayo kwa sasa hivi imeimarika zaidi, pamoja na Timu ya vollyboli katika shule ya wavulana ya Malaba ambayo ilishika nafasi ya kwanza katika mchezo huo. Mkuu wa shule hiyo alifurahia na kushukuru baada ya matokeo hayo. Ninapenda sana mchezo wa Voliball.
9. Nina matumaini makubwa kwamba Kenya inaweza kuenda mbali zaidi katika mchezo huu wa voli boli.
10. Ninaweza kusema unapokuwa na Hope, matumaini kila kitu kinawezekana. Ninapenda rafiki zangu wote ambao wanaishi nchini Kenya na ninaamini ya kwamba kuwasiliano na wenzako ni jambo muhimu. Ninaipenda Kenya na ninawenda wasikilizaji wote wa Idhaa ya Kiswahili ya Redio Japani. Pia niko na kasha la kuwekea msaada kwenye mgahawa kwa ajili ya kujenga sehemu ya kufanyia mazoezi nchini Kenya.