Rais Barack Obama amemtaja Donald Trump "wa ajabu" na "asiye na ufahamu" baada ya mgombea huyo wa Republican kusema kuwa rais wa Urusi Vradimir Putin ni kiongozi mzuri zaidi kuliko Obama.
Akizungumza Laos, Bw Obama amesema kuwa kila mara Bw Trump anapoongea inabainika kwazi kwamba mgombea wa Republican hafai kuwa rais.
Katika kipindi cha televisheni siku ya Jumatano, Bw Trump alimsifu Bw Putin kuwa ni "mtu mwenye uwezo mzuri wa kudhibiti mambo" na kumpa kiwango cha asilimia 82% cha uwezo huo.