Kila moja alirukia nyuma kwa mshangao. kuku alikasikira sana alipomwona Panzi.
Akamuuliza, "Nani alikwambia ukae hapo kichakani na kusikiliza mazungmuzo ya watu wengine?
wewe ni mgombanishi mkubwa sana wa watu. Ondoka hapa mara moja la sivyo, nitakudonoa na wewe pia."
Mara akatokea Kwavi kwenye kichaka kingine, akasema, "Hata mimi nilikusikia ukimwambia buibui kuwa aachane na Mwewe na matatizo yake. Kwa kweli mimi sikujua kama wewe kuku ni mkatili mkubwa. Yaani unamwambia Buibui aachane na Mwewe na matatizo yake ya kuuguliwa na watoto wake badala ya kwenda kumsaidia? Je, wewe kweli ni rafiki ya Mwewe? Urafiki gani huo? Kumbuka usemi usemao, rafiki wa kweli ni yule akufaaye katika dhiki. Je wewe umemfaa rafiki yako wakati wa dhiki ya kuuguliwa na wanawe?"
"Nyamaza!" Alifoka Kuku, "Huwezi kuniambia mameno kama hayo! Wewe ni mdudu mdogo sana kwangu. Hujui kuwa mimi nina uwezo wa kukudona hadi ufe? Mdudumdogo lakini una kelele nyingi!" Kuku na Kiwavi walipokuwa wakijibuzana hivyo, Mwewe akaelekea nyumbani kwake kuona hali ya watoto wake. Alipokaribia nyumba yake alisikia kelele za vilio. Akahisi kuwa mtoto mwingine alikuwa amefariki. Akiidhiwa nguvu kwa chungu. Rafiki zake walikuja kumlaki. Walimkumbatia, kisha walimwongoza hadi nyumbani. Kulikuwa kumejaa wadudu na ndege wengi.
Walimpa pole nyingi Mwewe."Tunajua kwamba huu ni msiba mkubwa sana lakini tumwachie Mungu. Kazi ya Mungu haina makosa!" Walimfariji.
Mwewe akauliza kwa huzumi, "Ni mtoto yupi tena aliyefariki?"
Wale marafiki wakaangakiana, kisha mmoja wao akajikaza akasema, "Si mtoto mmoja yu bali wote wametuacha. Pole sana ndugu yetu." Akanyamaza.
Hapo Mwewe hakuvumilia akaangua kilio.
Mwisho akasema, "kuku amemuua mganga Buibui, watoto wangu wote wamekufa. Buibui alikuwa na dawa za kuwaponya. Ubaya alionifanyia kuku ni mkubwa, sitausahau kamwe. Kuanzia sasa nikimwona kuku nitamkamata, Watoto wake watakuwa ni chakula changu!"
Tangu hapo urafiki wa Mwewe na Kuku ukaisha. Ukabaki uadui tu.
Kuku naye akiwaona Panzi na kiwavi huwadonoa na kuwaka, kwa sababu ashahidi wao ndio ulivunga urafiki kati yake na Mwewe.